Habari iliyoripotiwa hivi punde na vyombo vya habari vya kimataifa ni hii ya nchini Pakistan ambapo leo August 8 2016 kumetokea shambulio la kujitoa mhanga nje ya hospitali katika mji wa Quetta.
Imeelezwa
kuwa shambulio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kundi la watu wakiwemo
wanasheria na waandishi wa habari waliokuwa wakiusindikiza mwili wa
mwanansheria maarufu, Bilal Anwar Kasi, ambaye alipigwa risasi.
Takribani watu 120
wameripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea kwenye geti la
hospitali kwenye idara ya dharura ambapo mwili wa mwanasheria huyo
maarufu aliyepigwa risasi mapema jumatatu ulikuwa unaletwa hospitalini
hapo.
Majeruhi wanaotajwa ni wanasheria na waandishi wa habari ambao walikuwa wakiusindikiza mwili wa Bilal Anwar Kasi, bado haijajulikana aliyehusika katika shambulio hilo
Mji wa
Quetta umetajwa kuwa na mauaji ya mara kwa mara na kuuawa kwa wanasheria
wengi nchini hapo kwa kuhusishwa kwa kundi la waasi linaloshutumiwa
kufanya matukio hayo.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
No comments:
Post a Comment