Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo ambayeametua Msimbazi hivi karibuni, leo amefunga goli lake kwanza kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya mechi ambayo imemalizika kwa Simba kushinda magoli 4-0.
Mavugo ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Frederic Blagnon, ameonekana kuwavuruga mashabiki wa Simba kutokana na kiwa alichokionesha kwenye mchezo dhidi ya Leopards. Mavugo ame-assist goli moja ambalo lilifungwa na Shiza Kichuya kabla ya kufunga bao ambalo pia pasi ilitoka kwa Kichuya.
Ibrahim Ajib alianza kuifungia Simba bao la kwanza dakika chache kabla ya mapumziko lakini mfungaji huyo wa goli bora la ligi alifunga tena bao la pili katika kipindi cha pili. Kichuya alifunga bao la tatu huku Mavugo akihitimisha Simba Day kwa kupachika bao la nne.
No comments:
Post a Comment