Thursday, 18 February 2016

Besigye aachiliwa na polisi Uganda


  •     Image copyright BBC World Service                            
Msemaji wa chama cha Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye aliyekuwa amekamatwa na polisi sasa ameachiliwa huru.
Kanali huyo mstaafu ambaye ni kigogo wa upinzani nchini Uganda alikuwa amekamatwa katika kitongoji cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani, wakiambatana na kanali Besigye, wanadai walifumania watu wakiiba kura na wakataka usaidizi wa polisi kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.
Haijabainika alipelekwa wapi.
Hii na mara ya pili kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki hii.
Jumatatu, wiki hii alikamatwa alipokuwa akijaribu kupitia katika barabara moja mjini Kampala.
BesigyeImage copyright AP
Image caption Jumatatu polisi walisema walimzuilia kumlinda
Polisi walisema hakuwa na idhini ya kupitia eneo hilo kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment