Mshambuliaji wa Liverpool, Christian Benteke akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi timu yake ikiilaza 2-1 Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Selhurst Park, London. Bao lingine la Liverpool ambalo ilicheza pungufu baada ya James Milner kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 62 lilifungwa na Roberto Firmino, baada ya Joe Ledley kutangulia kuifungia Palace

No comments:
Post a Comment