Sunday, 6 March 2016

Mbwana Samatta kashuhudia kipigo cha timu yake dhidi ya Standard de Liege


Usiku wa March 5 Ligi Kuu ya Ubelgiji nchi ambayo inaongoza kwa viwango vya ubora wa soka duniani imeendelea kama kawaida kwa klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kushuka dimbani.
Genk inayochezewa na Samatta safari hii ilikuwa ugenini kucheza mechi ugenini dhidi ya klabu ya Standard de Liege inayoshika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji, Genk ambayo ipo juu ya timu hiyo katika msimamo wa Ligi imekubali kipigo cha goli 2-1.
2684527
Standard de Liege ilifanikiwa kujihakikishia kupata point tatu kwa magoli ya Ivan Santini dakika ya 48, ikiwa ni dakika sita zimepita toka Genk wapate goli la kuongoza kupitia kwa Nikolaos Karelis, lakini baadae Jean-Luc Diarra Dompe akawakatisha tamaa Genk ya kupata hata  point moja kwa kufunga goli la pili.
82799
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye ndio ameshuhudia timu yake ya KRC Genk ipoteze kwa mara ya kwanza toka ajiunge nayo, aliingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis aliyefunga goli la kwanza, Samatta hakupata nafasi ya kufunga kama mechi iliyopita dhidi ya Brugge.

No comments:

Post a Comment