Kiongozi wa muda
mrefu wa Zimbabwe Robert Mugabe amejibu kwa mzaha swali kuhusu mrithi
wake na kusema bado anaweza kurusha ngumi.
Rais Mugabe aliulizwa nani atakayemrithi wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.Kiongozi huyo ambaye amekuwa uongozini tangu 1980 ametimiza umri wa miaka 92.
"Mbona unamtaka mrithi?" alimwuliza aliyekuwa akimhoji.
Bw Mugabe, alisema hatastaafu katikati mwa muhula wake wa sasa, ambao ulianza 2013.
“Mbona nikubali kuendelea kuongoza iwapo nina maradhi au ninaugua au siwezi kuongoza?” aliuliza.
No comments:
Post a Comment