Sunday, 22 May 2016

Kwa wasichana: je, unapata tabu kuchagua zawadi ya mpenzi wako (boyfriend) kwenye siku yake ya kuzaliwa?

Kama kuna kitu wanaume hawajawahi kujua ni presha inayompata mtoto wa kike akiwa anamnunulia boyfriend au ndugu yake wa kiume zawadi, kama ya birthday, au zawadi kwa kuhitumu chuo na vitu kama hizo. Kiukweli  huwa ni presha ya hali ya juu. Na kama mtu sio mpenzi basi ndio huwa ni kazi mara mbili. Kununua zawadi kwa mwanamke ni raisi sababu wanawake wengi hupenda vitu vidogo dogo kama maua, makutano n.k.
Baada ya kuona hili ni tatizo nikaona si mbaya kama nitasaidia wadada wengi ambao wanapata tatizo la kununua zawadi kwa wapenzi wao au rafiki zako, na kwa wale walio zoea kuwa nunulia wapenzi wao nguo za ndani , soksi na Vitambaa ya mafua waachee. Wapo wanaume wanakerekwa na haya huwa hawasemi tu.
Kwanza unaweza angalia mpenzi wako /ndugu yako ni mtu  anaependa vitu gani je? ni mpenda michezo, mpenda filamu, mpenda vitabu, anapenda kusafiri na mambo kama hayo?  Kuna vitu raisi kabisa kufanya katika kununua zawadi kwa ndugu wa kiume /Mpenzi  na hizi ndo zawadi raisi kwa wanaume
Saa Ya Mkononi
saaa za mkononi
Kuwa makini wakati wa kuchangua saa ya mkononi, wanaume wanaojielewa hupenda kuvaa saa za Gharama , Saa nzuri inaweza elezea wasifu wa mtu hasa kwa mwanaume, huwezi vaa suti na saa ya sh.3000 , kwahiyo kama huna bajeti nzuri ya saa ni bora ukafanya vitu vingine.
Jezi Ya Mchezo Aupendao

Najua ulitegemea niseme jezi ya mpira wa miguu, kitu nilichogundua sio kila mwanaume ni mpenzi wa mpira wa miguu, japo wengi wao ni wapenzi wa mpira huo.  kuna wanaoependa michezo mingine, kama mpira wa kikapu, golf,clicket, nk   basi mfurahishe kwa kumnunulia akipendacho. ila itakuwa raisi zaidi kwa wapenda mpira  wa miguu au kikapu sababu jezi zao zinapatikana kiraisi katika maduka ya nguo za wanaume.
Kofia
kofia
Wapo wanaume wanapenda sana kuvaa kofia, wengine hawawezi kutoka njee bila kofia au kusafiri bila kofia, mfurahishe kwa kumnunulia kofia anazopenda sababu kofia pia ziko na staili tofauti , ila wengi wetu tunajua zile Baseball cape ambazo tunaziita tu Cap, lakini kuna  Ascot cap, Boater, Flat cap  hio ni chache tu. Ziko nyingine  nyingi.
Wallet
WALLET NA MKANDA
wanaume wameumbwa wasaidiwa na wanawake unaweza ukakuta mwanaume anatumia wallet imechoka mpaka ni aibu kuitoa mbele za watu na sio kama hawezi kununua wallet nyingine ila tu sababu ni wavivu mpaka wapate mtu wa kuwa sukuma kufanya vitu vingine. So mnunulie mpenzi wako au ndugu yako wa kiume wallet kama zawadi.
Mkanda
Moja kati ya vitu mtu akiangalia kwa mwanaume alie chomekea ni mkanda wake  na viatu, sasa kabla hajafika kwenye viatu mkanda muhimu. Mwanaume hata apendeze vipi kama amevaa mkanda umechanika chanika sijui umebanduka banduka inamshushia  sana heshima. Mi binafsi namchukulia mwanaume huyo  kama mchafu.
Viatu
VIATU
Tukiacha raba, na wenyewe tunaita simple, mnunulie mwanaume /mpenzi wako viatu vizuri hasa vya kuvaa ofisini.  Au kama sio mpenzi wa mitoko hiyo basi mnunulie aina ya viatu anavyopenda. Kama ni Vans, Nike, Adidas nk.
Games
plau
Baadhi ya wanaume wanapenda kucheza video games, kama playstation 4,na kama ni mpenzi wa vitu hivyo mnunulie sababu Video Games sio kwa watoto pekeake, Marafiki wengine wakikutana wakistarehe  hupenda pia kutumia muda wao kujifuraisha na video games pamoja na vivywaji
Zawadi zingine ambazo wadada wengi wamezoea  kama makukato,nguo za ndani, vitambaa vya jasho ,kitunza funguo ni zawadi ambazo unaweza ukawa unampa mpenzi wako mara kwa mara ila sio zawadi ya kumpa mtu wakati wa sikuyake muhimu kama siku yake ya kuzaliwa au Kuhitimu chuo N.k

No comments:

Post a Comment