Sunday, 7 August 2016

Video: MAN UNITED BINGWA NGAO YA JAMII

Man United-ngao ya jamii


Jose Mourinho ameanza kibarua chake Manchester United kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii baada ya Zlatan Ibrahimovic kupachika bao la ushindi dakika za lala salama kuishinda Leicester City kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Wembley.

Jesse Lingard ambaye alifunga goli kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace enzi za kocha Louis van Gaal, aliifungia United bao la kuongoza kabla ya mapumziko baada ya kukimbia umbali wa mita 40 na kuwavuka wachezaji wanne na kupasia kamba.
Mabingwa wa ligi ya England Leicester City walisawazisha kufatia makosa Marouane Fellaini kurudisha pasi fupi kwa beki wake lakini Jamie Vardy akauwahi na kumzunguka David de Gea kisha kufunga goli.
Lakini Ibrahimovic ambaye amesajiliwa katika kipindi hiki aliifungia bao Man United alipokutana na krosi ya Antonio Valencia na kuiunganisha kwa kichwa mpira uliomshinda golikipa wa Leicester Kasper Schmeichel.
Ngao ya Jamii katika namba:
  • 21:Idadi ya Ngao za Jamii ambazo Manchester United imewahi kutwaa
  • 20:Miaka ya Jesse Lingard akiwa mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufunga kwenye fainali ya FA Cup pamoja na mchezo wa ngao ya hisani tangu Eric Cantona alipofanya hivyo mwaka 1996.
  • 97:Hakuna mchezaji mwingine aliyegusa mpira mara nyingi zaidi ya kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater.
  • 3: washindi wa FA Cup wamefanikiwa pia kushinda Ngao ya Jamii kwenye misimu mitatu iliyopita.

No comments:

Post a Comment