Monday, 8 August 2016

Mfalme wa Japan aonyesha nia ya kuondoka madarakani, katoa sababu zake


Mtu wangu taarifa inayogonga vichwa vya habari kwa sasa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni hii ya Mfalme wa Japan kuonyesha nia ya kutaka kuondoka madarakani wakati katika sheria za nchi hiyo hakuna nafasi inayomruhusu mfalme kuondoka madarakani. 

Mfalme wa Japan Akihito amelihutubia taifa hilo kupitia runinga ambapo ameeleza kuwa ametaka kung’atuka kutokana na kwamba ana wasiwasi na umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.
japan 5
Wananchi wa Japan wakifuatilia hotuba ya mfalme
Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atatathmini kwa makini nia hiyo ya mfalme huyo. Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989, habari kwamba anataka kung’atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.
wananchi japan
Wananchi wakionekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza nia yake ya kung’atuka

No comments:

Post a Comment