Klabu ya Manchester United leo imeripotiwa kukamilisha upimaji wa afya wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast Eric Bailly katika kuelekea kukamilisha usajili wake kutoka Villareal.
Wengi wa wapenzi wa soka hawakuwa wanalifahamu jina la Eric Bailly kabla ya kuanza kuhusishwa na Man United mapema wiki hii. Basi tutumie makala hii fupi kumfahamu beki huyu kutoka Afrika Magharibi.
Mwanzo
Eric Bertrand Bailly alizaliwa eneo la Bingerville, Ivory Coast – sehemu sawa na aliyozaliwa mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony.
Kutusua
Kipaji chake kilionekana na mtalaam kutoka klabu ya Espanyol Emilio Montagut wakati wa michuano ya vijana yaliyoandaliwa na kampuni ya Kihispania ya Promoesport huko Burkina Faso.
Kuanza taratibu.
Ingawa aliwasili Cornella-El Prat mnamo December 2011, na kisha kuingia katika mfumo wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 wa Espanyol, ilikuwa miezi 10 kabla ya Bailly hajapewa kibali cha kufanya kazi. Baada ya hapo akasubiri miezi 10 mingine kupata nafasi katika kikosi cha kwanza mnamo October 2014. Mechi ya kwanza ya soka la ushindani ilikuwa akiwa na miaka 20, ilikuwa mechi ya La Liga vs Real Sociedad, Espanyol wakashinda 2-0.
Kupanda
Ndani ya kipindi cha miezi minne tangu alipocheza mchezo wa kwanza wa La Liga, tayari alishapata nafasi ya kusajiliwa na Villareal na pia kuisadia timu yake ya taifa katika michuano ya African Cup of Nations.
Uhamisho huo ulifanyika wakati Bailly akiwa kwenye michuano ya AFCON ambayo mwishowe walishinda ubingwa – akiwa ndio mchezaji mdogo zaidi kwenye kikosi cha Herve Renard, akiwa ametoka kupata nafasi kwenye kikoso cha timu ya taifa mwezi mmoja nyuma, Bailly alikuwa mmoja wa wafungaji penati waliofunga upande wa Ivory Coast katika mikwajuiliyoamua bingwa.
Ununuzi wa faida
Bailly aliwagharimu Villarreal kiasi cha £4.4 million alipohama kutoka Espanyol. Beki huyomwenye miaka 22 alinunuliwa kuja kuchukua bafasi ya Gabriel Paulista ambaye alienda kujiunga na Arsenal.
Atafaa kutumika kwenye Premier League
Akiwa na kimo cha urefu wa 6ft na staili ya kucheza kwa utulivu, Bailly anaendana na mahitaji ya nguvu ya PremierLeague. Alikuwa sehemu ya safu ya ulinzi ya Villareal ambayo iliruhusu magoli 35 tu katika mechi 38 na akachezamechi zote.
Nidhamu
Tatizo la Bailly nje na ndani ya uwanja itakuwa namna ya kumtuliza. Alipata kadi za njano 10 na moja nyekundu katika msimu uliopita waLa Liga, ikiwa atafanikiwa kuzilinda hasira zake basi atafanikiwa sana Uingereza
No comments:
Post a Comment