ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.
Amesema,
Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na
kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya
demokrasia.
Zitto
ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka
kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu
Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.
“Mambo
kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa
nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na
kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili
kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;
“Wanatia
woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa
kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali
juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.
“Kama
leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza
wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya
badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.
Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.
Jeshi
hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba,
wanasheria wa ACT-Wazalendo wataenda mahakamani ili kupata tafsiri
sahihi.
“Lakini
kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi
tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na
wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na
kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.
“Lazima
tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi
kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.
Steven
Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya
hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki
iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.
“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.
“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”
Mwakibolwa
amesema kuwa, kwa sasa si vema kueleza maswali aliyoulizwa kwa kuwa si
muda na wakati sahihi wa kuliongelea suala hilo sababu liko chini ya
upelelezi.
No comments:
Post a Comment