Wednesday, 8 June 2016

Eric Bailly awa beki ghali zaidi kwa Manchester United tangu Ferdinand



Manchester United wamekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast, Eric Bailly kutoka Villareal.
  Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na United kwa ada ya uhamisho isiyopungua paundi millioni 30 na kusaini mkataba wa miaka 4.
Wakati akitambulishwa kwa waandishi wa habari Bailly alisema: “Ni ndoto iliyokamilika kujiunga na Manchester United. Kucheza soka katika ngazi ya juu zaidi ndio jambo ambalo nimekuwa nataka siku zote.”
  Manager wa Man United Jose Mourinho alisema: “Eric ana uwezo wa kuwa mmoja wa wachezaji bora ulimwenguni.”
Bailly ameshacheza mechi 40 za La Liga, mechi 5 za kwanza zilikuwa akiwa na Espanyol.
Alijiunga na Villarreal kwa £4.4m mnamo January 2015 na kucheza kila mechi huku akiisadia timu yake ya Taifa kushinda ubingwa wa AFCON wiki kadhaa mbele.
Bailly ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mourinho tangu mreno huyo alipoqnza kazi Old Trafford.
Bailly anakuwa beki ghali zaidi katika historia ya Manchester United tangu ulipofanyika usajili wa Rio Ferdinand.

No comments:

Post a Comment