Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez amethibitisha kuwa yeye ni
mshambuliaji wa kiwango cha ulimwengu baada ya kuweka kambani mabao 40
kwenye ligi ya La Liga huku akitoa ‘assists’ 16 na kuwapa Barcelona
ubingwa wa 24 katika historia ya La Liga.
Straika huyo wa Uruguay, ambaye ametoa mchango mkubwa hasa pale timu
yake ilipokuwa inahitaji msaada wake, alimaliza msimu kwa kufunga
hat-trick iliyopelekea timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi
ya Granada na kuwaacha wapinzani wao wakubwa Real Madrid katika nafasi
ya pili.
Hat-trick hiyo ya Suarez ya Jumapili maana yake ni kwamba, amekuwa si tu kinara wa mabao La Liga bali pia Ulaya kwa ujumla; Anataraji kuchukua tuzo ya ufungaji bora Ulaya kwa mara ya pili katika maisha yake ya soka baada ya kufunga mabao 40 katika michezo 35 msimu huu.
Suarez (29) kwa mara ya kwanza alipata tuzo hiyo mwaka 2014 baada ya kufungana magoli na Cristiano Ronaldo wakati huo akiwa Liverpool akifunga magoli 31 na kuwa mfungaji bora pia wa EPL.
Suarez amekuwa ni mchezaji wa kwanza La Liga mbali ya Messi na Ronaldo kushinda tuzo ya ufungaji bora (Pichichi) tangu mwaka 2009.
Ukiwa msimu wa 2015-15 ukielekea ukingoni huku ukiwa umeisha kwa baadhi ya ligi, hii ndiyo orodha ya wafungaji 10 bora wa Ulaya msimu huu:

No comments:
Post a Comment