Diego Simeone ni kocha wa Atletico Madrid ambaye tarehe 28
Mei,atakiongoza kikosi chake kucheza fainali ya UEFA Champions League
dhidi ya Real Madrid. Mfahamu Diego Simeone kwa undani zaidi;
- FAMILIA YA MPIRA
Baba yake Carlos Alberto Simeone alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu
wa ridhaa. Kaka yake na mdogo wake wanacheza River Plate. Vile vile Dada
yao ni mmoja wa wakala wao.
- MAISHA YA SOKA
Diego Simeone alikuwa anacheza kama kiungo mkabaji na alianza maisha
ya mpira katika timu ya Velez Sarsfield nchini Argentina kisha akaenda
Sevilla, Inter Milan na Lazio ambako alipata mafanikio makubwa kwa
kushinda makombe 4 ndani ya mwaka mmoja. Mwaka 1994 hadi 1997
aliitumikia Atletico Madrid kisha kurudi tena mwaka 2003 hadi 2005.
- AMKUTA TORRES NAHODHA
Fernando Torres ni mmoja wa wachezaji tegemezi wa kikosi cha Atletico
Madrid kinachonolewa na Diego Simeone. Baada ya Simeone kurejea kwa
mara ya pili Atletico Madrid alimkuta Torres ndiye nahodha wa timu hiyo
baada ya kuwa mfungaji bora wa klabu kwa misimu miwili mfululizo.
Simeone alikaa kwa miaka miwili na kuelekea zake kwao Argentina na
Torres alienda zake Liverpool nchini Uingereza.
- AJIFUNGIA BAFUNI KWA NUSU SAA
Februari 16 mwaka 2006, Diego Simeone alicheza mechi yake ya mwisho
kama mchezaji. Baada ya mechi kumalizika Simeone alijifungia bafuni kwa
nusu saw akitafakari nini afanye baada ya kustaafu mpira. Ndipo
alipoamua kuwa kocha.
- AFANANISHWA NA ‘THE SPECIAL ONE’
Makeke yake na mbinu zake zimemfanya afananishwe na kocha wa Kireno,
Jose Mourinho. Hata kwa mafanikio kidogo kwa Simeone si haba sana
alifanikiwa kushinda makombe 2 ndani ya miaka mitatu nchini Argentina.
Mwaka wake wa kwanza kama kocha wa Atletico Madrid afanikiwa kushinda
kombe la Europa league.
No comments:
Post a Comment