Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi
Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao kati ya Serikali na wauzaji wa
Filamu za nje(Hawapo Pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam
.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw Tairo.
Mwenyekiti wa wauzaji wa filamu
za nje Bw Joseph Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa kikao baina
ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo kilichofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
: Baadhi ya wauzaji wa Filamu za
nje walioshiriki katika kikao kati yao na Serikali cha kubadilisha
sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini kilichofanyika leo jijjini
Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na: Shamimu Nyaki
Kufuatia kuwepo kwa Filamu nyingi
za nje zinazouzwa hapa nchini bila kufuata Sheria ya uuzaji wa kazi
hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata na
kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia kukuza na kutangaza filamu za
hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati alipokuwa
akizungumza na wauzaji wa Filamu hizo leo jijini Dar es Salaam.
Amewataka wauzaji hao kuwa na
mkataba pamoja wamiiki wa kazi hizo ili waweze kufanya biashara hiyo
kwa uhalali kwakua Serikali itawasaidia kusimamia utekelezaji wa
mikataba hiyo na kurahisisha utekelezaji wa sheria iliyopo.
“Lazima mfuate na kutekeleza
Sheria iliyopo kwakua mimi nipo hapa kuisimamia na kuhakikisha sheria
hiyo inatekelezwa”.Alisema Mhe.Waziri Nape.
Aidha katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Bi Joyce Fissoo ameongeza kuwa ni lazima wauzaji wa filamu hizo
kuhakikisha kuwa filamu wanazouza zimehakikiwa na bodi ya filamu pamoja
na COSOTA ili kudhihirisha ubora wa kazi hizo na viwango vya hapa
nchini.
“Ni lazima muhakikishe kazi
mnazouza zimeruhusiwa na Bodi ya filamu pamoja na COSOTA na zinafuata
madili ya hapa nchini’’.Aliongeza Bi. Joyce.
Ameongeza kuwa bodi ya Filamu
pamoja na COSOTA wapo tayari kuwasaidia kupata haki miliki ya filamu
hizo wanazouza kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kuruhusu filamu gani
inastahili kuuzwa na ipi haistahili kuwepo sokoni.
Uuzaji wa filamu za nje hapa
nchini umechangia kwa kiasi kikubwa filamu za hapa nchini kukosa soko
hali inayochangia kudidimia kwa sanaa hiyo hapa nchini ambayo inatoa
ajira nyingi kwa vijana.
No comments:
Post a Comment