Sunday, 20 March 2016

HII NI RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRICA


Azam FC Leo hii ikiwa kwao Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam imeichapa Bidvest Wits ya Afrika Kusini Bao 4-3 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Kwanza ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Ushindi huu umewafanya Azam FC watinge Raundi ya Pili kwa Jumla ya Mabao 7-3 kwa vile walishinda Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Afrika Kusini Bao 3-0.
Kwenye Raundi ya Pili, Azam FC wataivaa Klabu kigogo ya Afrika Espérance de Tunis hapo Mwezi Aprili.
 CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Pili
**Mechi kuchezwa Aprili 8-10 na Marudiano ni Aprili 19-20
Vita Club Mokanda [Republic of the Congo] v Sagrada Esperança [Angola]
MC Oran [Algeria] v Mshindi Kawkash Marrakesh/Barrack Young Controller
Azam [Tanzania] v Espérance de Tunis [Tunisia]
Zanaco [Zambia] v Stade Gabèsien [Tunisia]    
CS Constantine [Algeria] v Misr El-Makasa [Egypt]     
FC Saint-Éloi Lupopo au Al-Ahly Shendi v Al-Tripoli au Medeama               
FUS Rabat [Morocco] v SC Villa [Uganda]        
Atlético Olympic au CF Mounana v Africa Sports au ENPPI    
**Washindi wa Raundi hii watasonga Raundi ya Mchujo wakijumuishwa na Timu zilizotolewa Raundi ya Pili ya CAF CHAMPIONZ LIGI

No comments:

Post a Comment