Sunday, 20 March 2016

KIPA GIANLUIGI BUFFON AWEKA REKODI YA KUTOPIGWA BAO MUDA MREFU!







Gianluigi Buffon ameweka Rekodi mpya ya kwenda muda mrefu bila kutunguliwa Bao lolote katika Ligi ya Italy ya Serie A wakati Juventus ikiwatwanga Mahasimu wao wa Mjini Turin Torino Bao 4-1 hii Leo.
Buffon aliivuka Rekodi ya Kipa Sebastiano Rossi ya kwenda Dakika 929 za Gemu bila kufungwa hata Bao 1 ambayo aliiweka Msimu wa 1993/94 baada ya Leo kudumu Dakika 4 za kwanza za Mechi yao na Torino bila kupigwa Bao na hivyo kuvuka Dakika 929.
Hata hivyo, mapema katika Kipindi cha Pili, hatimae, baada ya Dakika 974 za kutofungwa Bao, Buffon aliruhusu Bao la Penati ya Andrea Belotti na kuwapa Torino Bao lao pekee.
Katika Mechi hiyo Bao za Juve zilifungwa na Paul Pogba, Sami Khedira na mbili za Alvaro Morata.
Ushindi huo umewafanya Juve wafikishe Pointi 70 wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Napoli ambayo Leo itacheza na Genoa.

No comments:

Post a Comment