Thursday, 17 March 2016

UEFA EUROPA LIGI - ALHAMISI USIKU: MAN UNITED KUIPIGA LIVERPOOL 3 OLD TRAFFORD NA KUSONGA?



ALHAMISI Usiku ni Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA EUROPA LIGI na Manchester United na Tottenham zote ziko Viwanja vya Nyumbani kwao vikidaiwa kushinda kwa ushindi wa kishindo ili kutinga Robo Fainali kufuatia vipigo katika Mechi zao za kwanza.
Tottenham, maarufu kama Spurs, wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.
Nako huko Old Trafford ni marudiano ya Mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino.
Takwimu muhimu:
-Man United na Liverpool zimekutana Jumla ya Mechi 166 za Ligi na Man United wanaongoza kwa ushindi wa Mechi 67 kwa 55 za Liverpool na kwenye Mechi za Vikombe vya England walivyokutana, Man United wameshinda 11 na Liverpool Mechi 7 tu.
-Uwanjani Old Trafford, Man United wameitandika Liverpool katika Mechi 4 zilizopita zote zikiwa za Ligi na kushinda Mechi 9 kati ya 10 zilizopita Uwanjani Old Trafford wakipambana na Liverpool.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Manchester United: De Gea; Darmian, Smalling, Rojo, Blind; Schneiderlin, Schweinsteiger; Memphis, Mata, Lingard; Martial
Liverpool: Mignolet; Clyne, Lovren, Sakho, Moreno; Milner, Henderson, Can; Firmino, Sturridge, Coutinho
REFA: Milorad Mažić (Serbia)
EUROPA LEAGUE - Raundi ya Mtoano ya Timu 16 -Marudiano:
**Kwenye Mabano Magoli Mechi ya Kwanza
**Saa za Bongo
2100 Bayer 04 Leverkusen Villarreal CF [0-2]
2100 Valencia CF Athletic Club [0-1]
2100 Lazio Sparta Prague [1-1]
2305 RSC Anderlecht v FC Shakhtar Donetsk [1-3]
2305 Sevilla FC v FC Basel [0-0]
2305 Tottenham Hotspur v Borussia Dortmund [0-3]
2305 SC Braga v Fenerbahce [0-1]
2305 Manchester United Liverpool [0-2]
**Marudiano Alhamisi Machi 17
KALENDA
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi

No comments:

Post a Comment