Thursday, 17 March 2016

Ben Pol ataja kolabo rahisi zaidi aliyowahi kuifanya,Je alifanya na msanii yupi na kwenye wimbo gani?

benpol2

Msanii wa R&B Tanzania,Ben Pol amesema kuwa katika kolabo zote alizowahi kuzifanya,kolabo ya Mama yeyoo ya G.Nako ndio ilikuwa rahisi kupita zote.
Ben Pol ameweka wazi zaidi ya kuingiza sauti studio hakuna kingine alichofanya kwani kila kitu G.Nako alikuwa amemaliza.
kusema kweli mimi sijashika peni yangu kuandika chochote kwenye ile chorus,kwa sababu G.Nako alikuwa ameshaiandika na melody zake na kila kitu na wimbo mzima ameshaurekodi,kwa hiyo yeye akaniambia tu utaimba hapa mpaka hapa,naweza kusema ndio kazi rahisi niliyowahi fanya” alisema Ben Pol japo alipata sifa nyingi sana kupitia chorus hiyo.
Source:Clouds Fm

No comments:

Post a Comment