Msanii wa bongo fleva toka WCB,Harmonize amesema kamwe haamini kama
kujihusisha na uchawi pamoja na ushirikina kunaweza kumsaidia msanii
kutusua kimuziki.
Akihojiwa kwenye kipindi kimoja cha Tv msanii huyo amesema kuwa yeye
anaamini Mungu na kipaji ndivyo vinaweza kumfanya mtu ang’are kisanii.
“Siamini kuwa uchawi una nafasi kubwa
kwenye muziki,ingekuwa hivyo basi watoto wa waganga ndio wangekuwa wana
hit peke yao,Mungu ndio kitu pekee cha kuamini pamoja na talent yako”
Source: The Base,ITV
No comments:
Post a Comment