Msanii mpya kwenye lebo ya WCB,RayMond amefunguka na kusema kuwa
alikutana na Diamond kupitia Maromboso ambaye alitaka atoe maoni yake
kwenye wimbo mmoja wa Diamond.
RayMond amesema kuwa kadri alivyokuwa akifanya kazi na Diamond kwa
kutoa mawazo yake ndipo Diamond alipoona kuwa yeye anaweza hivyo
kumwomba Babu Tale amsadie kwa kuwa Tip Top kuna wasanii wengi.
“Diamond alimwambia Tale kwamba anataka
kunisaidia,kwa sababu Tip Top kuna wasanii wengi,na WCB kuna msanii
mmoja ambaye ni Harmonizer,kwa hiyo aliamua kunichukua kwa sababu aliona
nina kitu”
Source:AyoTv
No comments:
Post a Comment