Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) , Magdalena Sakaya akionyesha picha ya mhanga wa vipigo zanzibar.
****
WAKATI
uchaguzi wa marudio ukitarajiwa kufanyika jumapili visiwani Zanzibar,
Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa haki za binadamu zimeendelea
kuminywa kwa kiasi kikubwa visiwani humo huku wafuasi wa chama hicho
wakilengwa zaidi.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) , Magdalena Sakaya, ameyasema
hayo leo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu
ya Ofisi za Chama hicho zilizopo Buguruni jijini hapa.
Magdalena
amesema kuwa Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ya
haki za binadamu hivyo mambo yanayotokea Zanzibar ni ya kushangaza na
hayapaswi kufumbiwa macho kwa ustawi wa Taifa.
Amesema
kuwa baada ya CUF kutangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi
wa marudio , wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakiishi kwa hofu huku
vikundi vya matukio ya uhalifu maarufu’mazombi’ yakipiga watu pasipo na
kuchukuliwa hatua zozote na vyombo vya usalama.
“Mara
kwa mara tumekuwa tukiwaambia jeshi la polisi kuhusiana na haya mazombi
ila cha kushangaza hadi leo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusiana
na kukamatwa kwa makundi hayo ya mazombi,”alisema.
Chama
hicho kimesema kuwa viongozi wao kadhaa wamekamatwa kwa nyakati tofauti
ambapo jana Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa -Hamad Masoud,
alikamatwa na kuwekwa kizuizini na Polisi baada ya kutoa taarifa ya
matukio mbalimbali yanayoendelea visiwani humo ambayo ni ya kinyume na
haki za binadamu.
“Jambo
la kushangaza kila tukio baya likitokea wanasingiziwa wafuasi wetu,
mara kwa mara wamekuwa wakikamatwa na tangu januari hadi sasa zaidi ya
wafuasi 60 wamekamatwa kwa madai ya kuhusika na uvunjifu wa amani,”alisema.
“Sisi tumeamua kujitoa kwenye uchaguzi huo ili wananchi wetu wawe huru na kuwaepusha kwenye vurugu, kwa hiyo
Chama
cha Mapinduzi kisiwalazishe wananchi kufanya mambo ambayo wenyewe
hawako tayari kuyafanya na kuyaona ni kinyume na Katiba, kwa sababu
uchaguzi huo wa marudio ni haramu.
“Asilazimishwe mbuzi kunywa maji wakati hana kiu,”alisema Magdalena na kuongeza kuwa wangetegemea uchaguzi huo kufanyika kwa amani baada ya kutangaza kujitoa mapema mwaka huu.
Magdalena
alisema kuwa yapo maeneo kadhaa visiwani humo wananchi wamepigwa
marufuku ya kutoonekana wakitembea kuanzia saa mbili usiku hatua
inayosababisha hata wengine kushindwa kwenda kufanya ibada.
Akizungumzi
kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ya kusema
kuwa hakuna watu wanaopigwa visiwani humo, Kiongozi huyo wa Chama
alipinga madai hayo na kusema kuwa ni hatari kuudanganya umma kwa
kuficha ukweli na kuacha watanzania wateswe.
Aliishauri
Serikali kuhakikisha kuwa usalama wa wananchi visiwani humo
unaimarishwa kwa kufuata misngi ya haki za binadamu na utawala bora, pia
ichukue hatua dhidi ya ‘mazombi’ ambayo yamekuwa yakiripotiwa kupiga
watu kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment