Thursday, 17 March 2016

HAYA NI MATOKEO YA JANA UEFA CHAMPION LEAGUE ARSENAL WALITIA ADABU MBELE YA BACA

MABINGWA Watetezi Barcelona na Bayern Munich Jana Usiku zimefuzu kuingia Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na kukamilisha idadi ya Timu 8 ya Raundi hiy baada kushinda Mechi zao za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 walizocheza kwao.
Huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain, Barcelona waliinyuka Arsenal 3-1 na kutinga Robo Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-1 baada ya pia kushinda Mechi ya Kwanza 2-0.

Magoli:
Barcelona 3
-Neymar (18'),
-Suárez (65'),
-Messi (88')  
Arsenal 1
Elneny (51')

Barcelona sasa wako njiani kuiga kile kilichofanywa na AC Milan Miaka ya 1989 na 1990 kwa kutwaa UCL mara mbili mfululizo.
Kwa Arsenal huu sasa ni mwisho wa Msimu wao labda wafanye miujiza kwenye Ligi Kuu England ambako wanashika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikibaki 9 kwao.
VIKOSI:
Barcelona: ter Stegen, Dani Alves, Mascherano, Mathieu, Jordi Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.
Akiba: Bravo, Turan, Bartra, Munir, Sergi Roberto, Aleix Vidal, Vermaelen.
Arsenal: Ospina, Bellerin, Koscielny, Gabriel, Monreal, Flamini, Elneny, Iwobi, Ozil, Sanchez, Welbeck.
Akiba: Macey, Gibbs, Mertesacker, Giroud, Walcott, Campbell, Coquelin.
REFA: Sergei Karasev (Russia).

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI:
-Real Madrid
-VfL Wolfsburg
-Paris St Germain
-Benfica
-Man City
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Bayern Munich

Huko Allianz Arena Jijini Munich, Bayern Munich walitoka nyuma kwa Bao 2-0 hadi Mapumziko na kupata Sare ya 2-2 na Juventus na hivyo kulazimisha Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30 na wao kupiga Bao 2 nyingine katika kipindi hicho na kuibuka kidedea ka Bao 4-2.

Magoli:
Bayern Munich 4
-Lewandowski (73'),
-Müller (91'),
-Thiago Alcántara (108'),
-Coman (110')       
Juventus 2
-Pogba (5'),
-Cuadrado (28')

Gemu hii ililazimika kwenda Dakika za Nyongeza 30 kwa vile kwenye Mechi ya Kwanza iliyochezwa Turin Nchini Italy zilitoka 2-2.
Kwenye Mechi ya Jana, Paul Pogba na Juan Cuadrado waliitanguliza Juve 2-0 lakini
Robert Lewandowski akafufua matumaini ya Juve kwa kufunga Bao la kwanza na katika Dakika ya 91 Thomas Muller akasawazisha na Gemu kwenda muda wa nyongeza.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Bayern walipiga Bao 2 kupitia Thiago and Kingsley Coman na kushinda 4-2.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

No comments:

Post a Comment