Kikosi cha APR kikiongozwa na kocha wao Nizar Kanfir kimewasili jioni
hii lakini mara baada ya kutua nahodha wao Jean Claude Iranzi akatema
mkwara kwamba ujio wao ni kuja kuwafunga Yanga.
Iranzi amesema kwasasa wameijua yanga katika mchezo wa kwanza
waliofungwa 2-1 na sasa ni zamu yao kupokea kipigo wakiwa kwao kutokana
na maandalizi waliyoyafanya kwao
“Yanga ni timu nzuri tunajua kwamba wao walitufunga kwetu zile ni
dakika 90 za kwanza sasa ni zamu yao nao kufungwa hatukuja kucheza
kukamilisha ratiba,”amesema Iranzi.
No comments:
Post a Comment