Mrch 19 igi kuu ya Vodacom Tanzania bara itaendelea kwenye viwanja tofauti kwa michezo mitatu kupigwa siku hiyo, licha ya kuwepo kwa mchezo wa kimataifa siku hiyo kati ya Yanga dhidi ya APR, mchezo wa ligi kati ya Coastal Union dhidi ya Simba ndiyo utakuwa na ‘kick’ siku hiyo kulingana na ugumu na umuhimu wake kwa timu zote mbili.
Simba itakuwa mgeni wa Coastal kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga uwanja wenye kila sifa ya timu vigogo kuacha pointi kwenye dimba hilo linalomilikiwa na chama tawala (CCM).
Unataka kujua kwanini nasema game hii ni ngumu na yenye ladha kuliko ile ya kimataifa kati ya Yanga na APR FC ya Rwanda? Twende pamoja hatua kwa hatua mwisho wa siku utajua nini namaanisha…
Mechi tano zilizopita za kila timu na matokeo yake
Simba SC
Mechi tano za Simba kabla ya kukutana na Coastal Union, Mnyama amefanikiwa kuchukua pointi 12 kutokana na kushinda michezo minne. Simba imepata pointi 12 huku ikifaniwa kufunga jumla ya magoli nane na yenyewe ikifungwa magoli matatu.
13/02/2016 Stand United 1-2 Simba
20/02/2016 Yanga 2-0 Simba
06/03/2016 Simba 2-0 Mbeya City
10/03/2016 Simba 3-0 Ndanda
13/03/2016 Simba 1-0 Tanzania Prisons
Coastal Unio
‘Wagosi wa Kaya’ wao wamepata pointi sita pekee kati ya 15 kutokana na kushinda mechi mbili huku wakiziacha pointi nyingine tisa kwasababu ya kupoteza michezo mitatu kati ya michezo mitano. Katika mechi tano, Coastal Union imefunga magoli matau tu wakati wavu wake ukitikiswa mara tisa.
14/02/2016 Coastal Union 1-0 Azam FC
21/02/2016 Mwadui 2-1 Coastal Union
05/03/2016 Mtibwa Sugar 3-0 Coastal Union
Coastal Union 1-0 JKT Mgambo
Kagera Sugar 4-0 Coastal Union
Head to head (Coastal Union vs Simba)
Simba haijapata matokeo mepesi mbele ya Coastal Union katika mechi saba zilizopita katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Simba haijawahi kuifunga Coasta kwa magoli zaidi ya matatu kwenye ligi. Katika mechi saba zilizopita, Simba imeshinda mechi mbili tu mbele ya Coasta. Coastal yenyewe imeshinda mhezo mmoja tun katika kipindi hicho huku timu zote zikitoshana nguvu mara nne. Rekodi ya timu hizi katika mechi zilizopita inaonekana hapa chini….
19/03/ 2016 Coastal Union vs Simba???
28/10/2015 Simba 1-0 Coastal Union
07/02/2015 Coastal Union 0-0 Simba
21/09/2014 Simba 2-2 Coastal Union
23/03/2014 Simba 0-1 Coastal Union
23/10/2013 Simba 0-0 Coastal Union
10/03/2013 Simba 2-1 Coastal Union
13/10/2012 Coastal Union 0-0 Simba
Coastal kiboko ya vigogo
Katika msimu huu 2015/2016 Coastal imekuwa timu ya kwanza kuzifunga timu za Azam na Yanga ambazo zilikuwa hazijafungwa kabla, uwanja wa Mkwakwani umekuwa mgumu kwa timu vigogo vya VPL mbele ya Coastal Union.
Ikiwa na hali mbaya Coastal Union iliweza kuondoka na pointi tatu mbele ya Yanga iliyo katika ubora katika kila idara, kisanga hicho kikaikuta Azam ambayo pia iliduwazwa kwa bao 1-0 kwenye uwanja huohuo.
Simba inakwenda kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wake dhidi ya Coastal Union kutokana na rekodi nzuri ya Mayanja ambaye amepoteza mchezo mmoja kati ya michezo 10 tangu alipoingia Msimbazi.
Wengi wanatarajia miujiza ya Coastal kama ilivyozishtua Azam na Yanga ambaz zote zilipewa nafasi kubwa ya kuifunga Coastal ambayo msimu huu imekuwa na mwendo sawa na ‘kikongwe’ aliyebeba mzigo unaomzidi uwezo.
Ugumu wa mchezo wa Coastal Union vs Simba unasababishwa na vitu vingi
- Nafasi za timu zote mbili kwenyemsimamo wa ligi
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 23 hadi sasa, pointi nne mbele ya Azam na Yange zilizocheza mechi 21. Simba inawania ubingwa wa VPL baada ya kuukosa kwa misimu mitatu iliyopita na tayari imejiweka kwenye mazingira mazuri ikiwa inaendelea kushinda michezo yake ya ligi. Itahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza ligi licha ya wapinzani wake kwenye kinyang’anyiro hicho kuwa nyuma yake kwa michezo kadhaa.
Coasta Union
Hawa jamaa wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi zao 19 baada ya kushuka uwanjani mara 23. Wanajua fika ushindi dhidi ya Simba utawafanya waongeze pointi tatu na kufikisha pointi 21 na huenda zikawafanya wasogee juu kwa nafasi kadhaa. Hivyo mchezo huu hautakuwa rahisi hata kidogo licha ya Simba kukutana na timu ya mwisho katika msimamo wa ligi.
- Jackson Mayanja
- Abdulhalim Humoud, Miraj Adam na Ibrahim Twaha ‘Messi’
Miraji amefunga magoli manne na ku-asissts magoli mawili huku magoli yake ya freekick dhidi ya Yanga SC na Azam FC yakichangia ushindi muhimu wakati Coastal ilipowaangusha wababe hao wa ligi. Humoud amekuwa muimili muhimu wa eneo la katikati kwenye timu hiyo wakati Messi akifanya vizuri akichezeshwa kama kiongo mshambuliji au winga.
Simba na Coastal zote zinahistoria ya kupata pointi kwenye mechi ngumu ndani ya mkwakwani Stadium
Coastal Union
Wao wanachagizwa na ushindi wao dhidi ya vigogo vinavyowania ubingwa msimu huu Yanga na Azam ambao msimu huu Coastal Union ndio imekuwa timu ya kwanza kupata pointi tatu dhidi ya timu hizo na imewea kufanya hivyo ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Simba ni miongoni mwa timu zinazowania ubingwa msimu huu je itanyolewa Mkwakwani kama Yanga na Azam au itavunja utawala huo wa Coastal mbele ya timu tatu za juu?
Simba
Imecheza mechi mbili msimu huu kwenye uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Mgamo JKT na African Sports na kufanikiwa kupata ushindi na kuondoka na ponti sita, sasa je Simba itaweza kuchukua pointi tisa kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa kuzifunga timu zote za tanga kwenye uwanja wao wa nyumbani?
No comments:
Post a Comment