Msanii wa bongo fleva Tunda Man amefunguka na kusema kuwa hakuwai
kufikiria kama muziki ungekuja kuwa kazi ya ndoto yake badala yake
alikuwa anajua atakuja kuwa mchezaji wa mpira wa miguu.
Tunda Man amesema kuwa amewahi kucheza timu moja na mastaa wakubwa
kwenye mpira kama Boniface Pawasa,Matola,Machupa na Emanuel Gabriel yeye
akiwa kama kipa.
“ndoto zangu zote zilikuwa kwenye mpira
niliamini ungenifikisha mbali,nilikuwa nakodishwa hadi timu za jeshi na
kila wikiendi nilikuwa silali nyumbani kwa sababu ya mpira” alisema Tunda Man
Source: Clouds
No comments:
Post a Comment