Tuesday, 15 March 2016

HAYA NI MATOKEO YA UEFA MICHEZO YA JANA MATOKEO YOTE HAPA


Image result for UEFA
Manchester City na Atletico Madrid zimefuzu kuingia Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, zikijumuika na Timu nyingine 4 zilizopita Wiki iliyopita baada ya Jana kucheza Mechi zao za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
City, wakicheza kwao Etihad, walitoka Sare 0-0 na Dynamo Kiev lakini wamefuzu kwa vile walishinda Mechi yao ya kwanza huko Ukraine Bao 3-1.
Licha ya kusonga Ulaya, ikiwa ni mara yao ya kwanza kabisa kutinga Robo Fainali ya UCL, City walipata pigo mapema kwa kuwapoteza Masentahafu wao wote Wawili kwenye Mechi hiyo, Nahodha Vincent Kompany na Nicolas Otamendi, ambao waliumia.
Nako huko Vicente Calderon, Jijini Madrid Nchini Spain, Atletico Madrid na PSV Eindhoven zilitoka Sare 0-0 kama ilivyokuwa kwa Mechi yao ya kwanza na hivyo kulazimika kucheza Dakika za Nyongeza 30 ambazo nazo hazikuzaa Goli.
Kwenye Meikwaju ya Penati, Atletico Madrid waliibuka kidedea kwa kushinda kwa Penati 8-7 baada ya kila Timu kufunga Penati zao zote 7 za kwanza na Luciano Narsingh wa PSV kupiga na kugonga mwamba Penati ya 8 wakati Juanran akiifungia Atletico na kuwapa ushindi.

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI:
-Real Madrid
-VfL Wolfsburg
-Paris St Germain
-Benfica
-Man City
-Atletico Madrid
Bado Timu 2

Mechi za mwisho 2 za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa Leo Usiku na tamu kabisa ni ile ya Nou Camp wakati Barcelona wakirudiana na Arsenal huku wao wakiwa washindi wa 2-0 baada ya Mechi ya kwanza iliyochezwa Emirates.
Nyingine ni huko Allianz Arena Jijini Munich huku Bayern Munich na Juventus zikiwa zimetoka Sare ya 2-2 kutoka Mechi ya kwanza iliyochezwa Turin Nchini Italy.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
JUMANNE 15 MAR 2016
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili
Atletico Madrid 0 PSV Eindhoven 0 [0-0, Penati 8-7]
Man City 0 Dynamo Kiev 0 [3-1]  
JUMATANO 16 MAR 2016
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]

TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

No comments:

Post a Comment