Rapper Darassa kupitia video yake ya Kama Utanipenda ameweza kupata shavu la video hiyo kuruka kwenye kituo cha televisheni cha kimataifa cha Trace Tv wiki chache zilizopita.
Licha ya mafanikio hayo Darassa amesema bado hajafikiria kufanya kazi na msanii yeyote wa nje ya Tanzania kwa kuwa yeye ndoto yake kubwa ni kuwafanya watu wa nje wamtafute yeye kufanya naye kazi.
“mimi plan yangu sio kuwaza kufanya kazi na nani,ndoto zangu kubwa ni kuwafanya kina nani waweze kufanya kazi na mimi,kwa hiyo nina kazi ya kuutengeneza muziki wangu ili mtu mwingine ahitaji kufanya kazi na mimi” alijibu Darassa baada ya kuulizwa iwapo video yake kuchezwa Trace Tv italeta kolabo ya kimataifa.
Source: Radio 5
No comments:
Post a Comment