MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger, ambayo Timu yake Leo iko huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kurudiana na Miamba ya Soka Duniani FC Barcelona katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakiwa wamepigwa 2-0 katika Mechi ya kwanza, amejitokeza na kutetea rekodi yake Klabuni.
Kufuatia kufungwa 2-1 na Watford Jumapili iliyopita Uwanjani Emirates na kutupwa nje ya FA CUP, Kombe ambalo walilibeba kwa Misimu Miwili iliyopita, Mashabiki wa Arsenal walimtaka Wenger afungashe virago vyake na kutimka.
Hali hiyo pia imekuja baada ya Arsenal kujikuta wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City wakati walikuwa wakienda vizuri tu mwanzoni mwa Msimu.
Akiongea na Wanahabari huko Barcelona kuhusu Mechi yao ya Leo, Wenger alibaki kuitetea rekodi yake Klabuni Arsenal tangu ajiunge nao Mwaka 1996.
Alisema: “Nimeijenga Klabu kwa kufanya kazi kwa bidii, bila msaada wowote toka nje, na ukichukulia wapi tulipo Leo na tulipokuwa nilipoingia, utaona tumesonga mbele na tena bila ya pesa toka kwa Mtu yeyote bali kwa pesa za jasho letu!”
Aliongeza: “Tatizo ukikaa sehemu muda mrefu Watu wanahoji utumishi na uwezo wako lakini mie sina wasiwasi na natumia muda wangu mwingi kwa Klabu na nina motisha kubwa!”
Alipoulizwa kama anakerwa kupondwa na Mashabiki, Wenger alijibu: “Sitaki kuingia kwenye mjadala huo kwani unaweza kutafsiriwa kwa namna mbili.”
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI:
-Real Madrid
-VfL Wolfsburg
-Paris St Germain
-Benfica
-Man City
-Atletico Madrid
**Bado Timu 2
Leo Arsenal wana kibarua kigumu huko Nou Camp kupindua kipigo cha Bao 2-0 cha Mechi ya kwanza watakaporudiana na Barcelona ambao ni Mabingwa wa Spain, Ulaya na Dunia.
Tena hili limekuja wakati Arsenal wameshinda Mechi 1 tu kati ya 7 zilizopita lakini Wenger anaamini matokeo mema huko Nou Camp hii Leo yatawapa kiki ya kurejesha mbio zao za Ubingwa huko England.
Wenger ameeleza: “Tumepita kipindi kigumu hivi karibuni kutokana na matokeo yetu lakini muhimu ni kutulia na kuwa na nguvu. Nimecheza Mechi 200 za UCL na tumeshinda kila sehemu Ulaya isipokuwa hapa. Kesho [yaani Leo] tuna nafasi ya kufanikisha hilo!”
TATHMINI-BARCELONA v ARSENAL
>>LEO NOU CAMP, JIJINI BARCELONA, SPAIN
Katika Mechi ya kwanza huko Emirates, Bao 2 za Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, ndizo ziliwapa Barca ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Robo Fainali ya UCL.
Mechi zao zilizopita za Wikiendi:
Barcelona 6-0 Getafe (Juan Rodríguez 8 Kajifunga, El Haddadi 19, Neymar 32 51, Messi 40, Arda Turan 57)
-Ushindi huu umezidi kuwachimbia Barca kileleni mwa La Liga.
Arsenal 1-2 Watford (Ighalo 50, Guedioura 63; Welbeck 88)
-Kipigo hiki kiliwatupa Arsenal nje ya FA CUP ambayo wao walikuwa Mabingwa Watetezi kwa Misimu Miwili iliyopita.
VIKOSIN VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona: Ter Stegen; Alves, Mathieu, Mascherano, Alba; Busquets; Rakitić, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar.
Hawatacheza: Rafinha (Goti), Sandro (Musuli), Piqué (Kifungo)
Arsenal: Ospina; Bellerín, Mertesacker, Gabriel, Monreal; Coquelin, Elneny; Campbell, Özil, Sánchez; Giroud.
Hawatacheza: Ramsey (Paja), Čech (Musuli), Cazorla (Kifundo cha Mguu), Oxlade-Chamberlain (Goti), Rosický (Paja), Wilshere (Mguu)
Hatihati: Koscielny (Tatizo la Mguu)
REFA: Sergei Karasev (Russia)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili
Atletico Madrid 0 PSV Eindhoven 0 [0-0, Penati 8-7]
Man City 0 Dynamo Kiev 0 [3-1]
JUMATANO 16 MAR 2016
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]
TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
No comments:
Post a Comment