Saturday, 9 January 2016

LUKUVI AKABIDHI BATI ZA TSH MILIONI 4



Karibu wa mbunge jimbo la Ismani Bw Thom Malenga akikabidhi msaada wa bati 170 zenye thamani ya Tsh milioni 4.2 kwa diwani wa Malengamakali Bi Franzisca Kalinga leo
MBUNGE wa jimbo la Ismani mkoani Iringa Bw Wiliam Lukuvi amekabidhi msaada wa mabati 170 yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 4 .2 kisaidia Ujenzi wa vyumba vya madarasa na Bweni  jimboni.

Huku akiwataka wananchi kuendelea kushiriki shughuli za Ujenzi wa vyumba vya madarasa na Nyumba za walimu Kazi kubwa kuwaunga mkono .

Lukuvi ambae ni Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi alisema kuwa serikali ya Rais Dr John Magufuli imewapunguzia mzigo wazazi  nchini kwa kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari ili kuwafanya wananchi kuondokana na Kero hiyo.

Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya mbunge Lukuvi , Katibu wake Bw Thom Malenga alisema msaada huo umetokana na maombi ya wananchi wa kata ya Malenga Makali kupitia diwani wake Bi Franzisca Kalinga .

Kuwa bati hizo zitakwenda shule ya msingi Isaka ambao wamejenga ma jengo mawili ya shule na walikwama bati 70 zenye thamani ya zaidi tsh milioni 1.7 wakati bati nyingine zitakwenda shule ya sekondari Nyerere ambao jengo la  bweni limekamilika na wanahitaji bati 100 zenye thamani ya zaidi ya tsh milioni 2.5

Hivyo aliwataka wananchi hasa viongozi kusimamia vema matumizi ya bati hizo ili ziweze kutumika kwa shughuli husika na si vinginevyo.

Aliwataka wananchi kuendelea na Ujenzi wa Nyumba za walimu pamoja na vyumba vya madarasa na kuwa mbunge Lukuvi atandelea kuwaunga mkono pale wanapokwama .


Diwani wa kata ya Malengamakali Bi Franzisca Kalinga mbali ya kumpongeza Mbunge Lukuvi kwa msaada huo bado alisema msaada huo punguza Kero ya wananchi kuchangishana Pesa za bati 

Kwani alisema kata yake ni moja ya kata zinazokabiliwa na tatizo la ukame kwa kuwa na njaa hivyo bila msaada huo wa mbunge na majengo hayo yangeweza kusimama.

No comments:

Post a Comment