Saturday, 9 January 2016

Davido amaliza tofauti zake na Mama wa mtoto wake

Ugomvi wa mwanamuziki wa Nigeria, Davido na mama wa mtoto wake Sophia Momodu umekwisha.
dav
Familia hizo mbili zimefanya mkutano wa makubaliano ya malezi ya mtoto wao na pia wamekubaliana kutogombana kwenye mitandao ya kijamii, Pia Sophia Momodu pia amepewa haki za kumtembelea mtoto wao anayeishi na dada yake Davido ‘Ashley Adeleke’.
Mkutano ulihudhuriwa na Sophia,baba mzazi wa Davido Deji Adeleke, Bwana na Bibi Dele Momodu na wakili wao.
Familia hizo mbili ziliingia kwenye vita kubwa ya malezi ya mtoto wao baada ya Sophia kudai kuwa Davido na famili yake walikua wamepanga kumtorosha mtoto wake nje ya nchi bila ruhusa yake.

No comments:

Post a Comment