Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote,
wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza usiku saa 8
uwanja wa ndege wa JK Nyerere kumpokea mchezaji bora wa Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ndani Mbwana Samatta.
Baada
ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerere, Samatta alipokelewa na
viongozi wa serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na mama yake mzazi
na watanzania wengi walijitokeza kumlaki mchezaji huyo.
Mara
baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF ilimpeleka moja kwa moja
kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta jijini Dar es
salaam, ambapo imemlipia gharama ya kukaa kwa siku mbili.
Akiwa
hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo, Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda alitoa salamu
za pongezi kwa niaba ya Serikali, kisha mchezaji alipata nafasi ya
kuongea na waandishi wa habari.
Kwa
kuwa Jumanne, Januari 12 ni Sikukuu ya Mapinduzi, na Janauri 13 ni
fainali ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, siku ya Alhamisi
Januari 14 TFF imeandaa dua maalumu ya kumpongeza Samatta itakayongozwa
na viongozi wa dini mbalimbali katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11
jioni.
Hata
hivyo ratiba zingine za kumpongeza Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa
na wadau wengine zinaweza kuendelea ilimradi TFF ijulishwe mapema kwa
ajili ya kuratibu uwepo wa mchezaji mwenyewe.
No comments:
Post a Comment