Tuesday, 9 August 2016

GOLIKIPA MTANZANIA ANAYECHEZA LIGI KUU MSUMBIJI AVUNJIKA MKONO

IMG_201608223_120829




MLINDA mlango wa zamani wa JKT Oljoro, Bady Abdul ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa katika timu ya Chingari de Tete ya ligi kuu Msumbiji amevunjika mkono wake wa kulia na atasubiri hadi Septemba 2 kujua maendeleo yake.

Mlinda mlango huyo ambaye amejiunga na Chingari hivi karibuni alikuwa tayari amejihakikishia namba katika timu hiyo iliyo nafasi ya 13 katika ligi yenye timu 16.

“Bado mechi kumi ligi imalizike,” anasema Bady nilipofanya naye mahojiano Jumanne hii akiwa nchini Msumbiji.
“Tumecheza game 20, mimi nimejiunga hapa hivi karibuni na hadi naumia nilikuwa nimeshacheza mechi 6. Kwa sasa naendelea vizuri na daktari ameniambia tarehe 2 mwezi ujao naweza kuondoa plasta ngumu-P.O.P,” anasema kijana huyo mwenye miaka 22.

No comments:

Post a Comment