USIKU wa kuamkia jana, Saa 8 na Nusu kwa Saa za Bongo, Manchester United, ilitoa Video rasmi kumtangaza rasmi Paul Pogba kurejea Klabuni hapo kutoka Juventus ya Italy baada ya Dili ya Uhamisho wake kukamilika.
Pogba, mwenye Miaka 23, amesema ‘Huu ni wakati muafaka kurejea Old Trafford’ baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitano kwa Uhamisho wa Ada ya Pauni Milioni 89 ambayo ni Rekodi ya Dunia.
Sasa ni Miaka Minne tangu Pogba aihame Man United na kwenda Juventus kwa gharama ya Pauni Milioni 1 na Nusu.
Baada ya kusaini Mkataba, Pogba alisema: “Hii ni Klabu sahihi kwangu kupata mafanikio yote ninayotegemea!”
Nae Meneja wa Man United, Jose Mourinho, amesema: “Pogba anaweza kuwa ndio moyo wa Klabu kwa Miaka 10 ijayo!”
Dau la Uhamisho wa Pogba limezidi ule Uhamisho ulioshika Rekodi Duniani wa Mwaka 2013 wa Gareth Bale kuihama Tottenham Hotspur na kwenda Real Madrid kwa Pauni Milioni 85.
Pogba akiwa na Juventus aliisaidia Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Serie A katika kila Mwaka katika Misimu yake yote Minne aliyokuwa huko.
Chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho, Pogba anakuwa ni Mchezaji wa Nne Mpya kusainiwa na wengine ni Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.
Pogba alijiunga na Man United Mwaka 2009 akiwa na Miaka 16 tu kutoka Klabu ya France Le Havre na kuhamia Juve ambako alicheza Mechi 178 na kufunga Bao 34.
Pogba ameeleza kuwa Mama yake Mzazi alimwambia atarudi tu Old Trafford kwani hayo ndiyo ‘hatima’ yake.
Akiongea na MUTV, Pogba ameeleza: “Ndio kwanza nimerudi Carrington. Ni kama nimerudi Nyumbani. Nilikwenda tu Likizo!’
POGBA – Mafanikio yake:
U-20 Kombe la Dunia na Mchezaji Bora (2013)
4 Ubingwa Serie A (2013, 2014, 2015, 2016)
2 Copa Italia (2015, 2016)
2 Italia Super Cup (2014, 2015)
UHAMISHO – Rekodi za Dunia za hivi karibuni:
2013 - Gareth Bale £85m (Tottenham Hotspur kwenda Real Madrid)
2009 - Cristiano Ronaldo £80m (Manchester United kwenda Real Madrid)
2009 - Kaka £56m (AC Milan kwendaReal Madrid)
2001 - Zinedine Zidane £46m (Juventus kwenda Real Madrid)
2000 - Luis Figo £37m (Barcelona kwenda Real Madrid)
No comments:
Post a Comment