Diamond aliongea hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika na kusema kuwa beef husaidia kutengeneza ‘attention’ na hivyo kusaidia tasnia ya muziki kukua vizuri akitolea mfano muziki wa hip hpo wa marekani ulivyokua kutokana na bifu za 2 Pac na Biggie na bifu ya Jay z na Nas na kuongeza kuwa hata watanzania walimfahamu sana WizKid baada ya bifu yake na Davido
“Wakati mwingine haya masuala ya bifu hayana madhara kwa sababu yanasaidia kwa namna nyingine kupenya,kwa hiyo ni namna ya kuangalia tu sisi wenyewe tufanye namna gani hili bifu lisiingie kwenye familia na watu wengine tukaanza kulogana,lakini kwenye muziki liwepo ili kutengeneza attention zaidi Afrika,watu waangalie kuna nini,inasaidia industry kukua haraka” alisema Diamond na kusisitiza kuwa bifu hizo zisivuke mpaka kwenye maisha ya kawaida.
No comments:
Post a Comment