Wednesday, 17 August 2016

AZAM YABEBA NGAO YA JAMII KWA KUICHAPA YANGA

IMG_0401

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga SC imenyang’anywa Ngao ya Jamii na Azam FC baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-1 kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 2-2 katika mchezo huo ambao ni wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara 2016/17.

IMG_0308
Yanga ambao walikuwa wakiishikilia Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam kwenye mchezo wa msimu uliopita kwa changamoto ya mikwaju ya penati, walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kubeba tena ngao hiyo hiyo kutokana na kuongoza mchezo huo kwa magoli 2-0 yaliyofungwa kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alifunga bao la kwanza dakika ya 20 kwa njia ya penati kufuatia yeye mwenyewe (Ngoma) kuanngushwa kwenye box na beki wa Azam David Mwantika.
IMG_0279
Dakika moja baadaye, Ngoma akaifungia tena Yanga bao la pili akiunganisha pasi ya Amis Tambwe ambaye alitumia vizuri makosa ya Mwantika aliyeshindwa ku-control mpira na kunyang’anywa na Tambwe.
IMG_0391
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zikamalizika kwa Yanga kuwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC.
Dakika ya 74 Shomari Kapombe aliipatia Azam bao la kwanza akitumia makosa ya mabeki wa Yanga waliozembea kuondosha mpira kwenye eneo la hatari la goli lao.
IMG_0323
John Bocco ‘Adebayor’ aliisawazishia Azam kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 penati iliyotokana na beki wa Yanga kuushika mpira kwenye box.
IMG_0317
Penati za Azam ziliwekwa kambani na John Bocco, Himid Mao, Shomari Kapombe na Michael Balou.
IMG_0313
Deogratius Munishi ndiye mchezaji pekee aliyefunga penati kwa upande wa Yanga huku Hassan Kessy akishuhudia penati yake ikidakwa na golikipa wa Azam Aishi Manula wakati Haruna Niyonzima yeye penati yake iligonga ‘mtambaa panya’ na kutoka nje.
IMG_0362
Katika kipindi cha miaka mitano ya hivi karibuni, Azam na Yanga zimekutana mara nne mfululizo kuwania Ngao ya Jamii huku Yanga wakiongoza kuinyakua mara nyingi zaidi ya wapinzani wao.
Yanga wametwaa ngao hiyo mara tatu (mara zote kwa kuifunga Azam) huku ushindi wa leo ukiwapa Azam ngao hiyo kwa mara ya pili.

No comments:

Post a Comment