Wednesday, 1 June 2016

Sentensi 3 za Jose Mourinho baada ya kuulizwa kuhusu upinzani wake na Pep Guardiola

Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2016/2017 unatarajiwa utakuwa moja kati ya msimu unaovutia zaidi Uingereza, hiyo inatokana na Jose Mourinho kujiunga na Man United lakini pia Pep Guardiola kujiunga na Man City, upinzani wa makocha hao ulianzia Hispania mmoja akiifundisha FC Barcelona na mwingine akiifundisha Real Madrid.
Upinzani wa makocha ulianzia Hispania ila unatarajiwa kurudi Uingereza baada ya wote kujiunga na vilabu vyenye upinzani mkubwa na vinatokea jiji moja la Manchester, Jose Mourinho leo May 31 2016 alifunguka na kueleza mambo kadhaa kuhusu upinzani wao na Gurdiola utaendelea?
“Kilichotokea miaka miwili iliyopita hakinifanyi mimi kuwa na hatia, miaka miwili mimi na Pep tuliakuwa katika Ligi moja Ubingwa ilikuwa achukue yeye au mimi, kwa hali kama hiyo upinzani wangu binafsi na yeye lazima uendelee kwa sababu utakuwa na maana fulani katika Ligi Kuu Uingereza”

No comments:

Post a Comment