Rais wa Burundi
Pierre Nkurunziza amewapatia waasi makataa ya wiki mbili
kujisalimisha.''Iwapo hawatasalimu amri nitakabiliana nao kwa nguvu''.
Rais
alitoa matamshi hayo wakati wa ziara yake katika mji wa Mugamba yapata
kilomita 80 kusini mwa mji wa Bujumbura ambao umetajwa kuwa na makundi
mengi ya waasi.Ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia mbinu kama hiyo zilizoangamiza maandamano dhidi ya serikali mwaka 2010 ambayo mashirika ya kibinaadamu yanasema yalihusisha unyanyasaji mkubwa.
Burundi imekabiliwa na ghasia za kisiasa za mda mrefu tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 400 wamefariki tangu kuanza kwa mgogoro huo mnamo mwezi Aprili 2015 na takriban watu 260,000 wametoroka taifa hilo.
No comments:
Post a Comment