Thursday, 2 June 2016

Staa wa kwanza kusajiliwa na Pep Guardiola Man City ametangazwa leo June 2 2016


Klabu ya Manchester City ya Uingereza leo June 2 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa kwanza wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani aliyekuwa anaichezea klabu ya Borrusia Dortmund Ilkay Gundogan.
Man City wametangaza kumsajili Ilkay Gundogan kwa mkataba wa miaka minne lakini ada ya usajili ya nyota huyo inakadiliwa kufikia pound milioni 21 ambazo ni zaidi ya bilioni 60 za kitanzania.
34D8107500000578-0-image-a-1_1464855462585
Ilkay Gundogan ambaye ni kiungo wa kati, ana umri wa miaka 25 , lakini hadi anaondoka Dortmund na kujiunga na Man City alikuwa kacheza jumla ya mechi 157, lakini katika msimu uliomalizika wa Bundesliga, Ilkay Gundogan amecheza mechi 25, kafunga goli moja, katengeneza nafasi 26 za magoli na kupiga pasi zilizofika kwa wastani wa asilimia 39.
ALL GOALS: Azam FC Vs Esperance ya Tunisia April 10 2016 (Full Time 2-1)

No comments:

Post a Comment