Monday, 6 June 2016

AUDIO: Kauli ya Jerry Muro baada ya kupeleka vielelezo TAKUKURU kuhusu wanaohujumu Yanga

siku chache zimepita toka mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amuagize mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro apeleke vielelezo TAKUKURU, kuhusu watu wanaosadikiwa kupanga njama za kuhujumu uchaguzi wa Yanga hususani Yusuph Manji, Jerry leo amewasilisha vielelezo TAKUKURU.
“Leo tumetekeleza maelekezo ya yaliotolewa na mwenyekiti wetu, kwanza kuwasilisha tuhuma zote zilizotolewa na mwenyekiti wetu tunaziwakilisha TAKUKURU, kama unakumbuka katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kuchukua fomu alitoa maelekezo hayo na sisi tumetekeleza”


No comments:

Post a Comment