Sunday, 29 May 2016

Sokwe auawa baada ya kumshika mtoto Marekani


Wafanyikazi wa hifadhi moja wa wanyama nchi Marekani wemempiga risasi na kumuua sokwe mmoja baada ya mtoto mmoja kuingia kwenye hifadhi hiyo.
Mkurugenzi wa hifadhi Cincinnati, alisema kuwa mtoto huyo mvulana wa umri wa miaka minne, alitambaa na kupita kuzuizi na kisha kuanguka kwenda mahala alikuwa sokwe huyo kwa jina Harambe, ambaye alimshika na kuanza kumburuta.
Aliitaja hatua ya kumuua sokwe huyo kama uamuzi mgumu lakini ulio muhimu. Mtoto huyo hakupata majeraha mabaya.

No comments:

Post a Comment