Klabu ya Real Madrid ya Hispania usiku
wa May 28 2016 ilicheza mchezo wake wa fainali ya Klabu Bingwa barani
dhidi ya Atletico Madrid katika jiji la Milan Italia uwanja wa San Siro,
hiyo ilikuwa fainali inayohusisha timu kutoka jiji moja la Madrid,
hivyo upinzani ulikuwa mkubwa.
Katika mchezo huo wa fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, Real Madrid walifanikiwa kutwaa Kombe lao 11, huku
Atletico wakiambulia kushindwa kuweka rekodi ya kutwaa Kombe hilo kwa
mara ya kwanza katika historia ya klabu yao, Real Madrid walifanikiwa
kuifunga Atletico kwa mikwaju ya penati 5-3, hiyo ni baada ya dakika 12o
kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Baada ya Ubingwa Real Madrid waliwasili Hispania katika jiji la Madrid wakiwa na Kombe lao la 11 la UEFA.
No comments:
Post a Comment