boti |
Umoja wa mataifa
unasema kuwa huenda wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika
kipindi cha siku tatau zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Msemaji
wa Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi, Carlotta
Sami, amesema kuwa mashua kadhaa yalizama katika maeneo ya kusini mwa
Italia Jumatano usiku ikiwa na wahamiaji hao.Wahamiaji waliokololewa juma lililopita kutoka katika boti moja kwenye bahari ya Mediterranea, wamewaambia wafanyikazi wa makundi ya uokoaji kuwa, waliona chombo kimoja cha baharini kilichojaa wakimbizi kikizama.
Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jana Jumamosi.
Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.
No comments:
Post a Comment