Mapenzi yanaumiza sana, na kabla hujaanza kuwaza kumtokea
msichana mwingine au wewe dada kumkubali Yule mshikaji alikuwa
anakufwatilia kwa mwaka sana, fanya haya yafwatayo
Jipende kuliko Kawaida
Tumia muda huu ambao uko single na ujipende zaidi kuliko ulivyokuwa
katika mahusiano, muda wa kujiwaza wewe, kula vizuri, vaa vizuri, pata
muda mwingi wa kupumzika, tembelea sehemu za starehe mwenyewe bila
kuwaza kutafuta mtu mwingine na utajifunza kitu.
Kuna na Marafiki wa jinsia tofauti na wewe
Jichanganye na marafiki wa jinsia tofauti na wewe na ujifunze mambo
ya mahusiano kupitia kwao, toka nao matembezini au sehemu za michezo ila
usianze mahusiano mapema kama hauko tayari.
Kuwa Karibu na Ndugu zako
Huwezi jua ni kwa kiasi gani umekaa mbali na watu wako wa karibu
wakati ukiwa uko busy na mpenzi wako. Wakati kama huu utumie kutoka na
ndugu zako wa karibu au kushinda nyumbani mwisho wa wiki, pamoja na
familia yako.
Fanikisha Ndoto zako
Ukiwa katika mahusiano kila kitu lazima kiwe kwa ajili ya wote wawili
ila kama upo single ni raisi kufanya kitu kwa ajili yako mwenye na
tumia muda huu kufanikisha ndoto zako, fikiria malengo yako zaidi ili
ufanikiwe.
Tafakari nini unataka kwenye Mahusiano Mengine
Tumia huu muda, kuangalia ni aina gani ya mpenzi unamuhitaji na nini
kitakupa furaha kutoka kwake, ila pia tambua furaha kama haipo kwako
huwezi tegemea kuipata kwa binadamu mwingine. Kwahiyo jua ni jinsi gani
utakuwa na furaha bila kutegemea mapenzi au kuwa na mpenzi.
Fanya kitu kipya
Kama kufuga mbwa ,paka au chochote ambacho hujawahi fanya hakikisha
haukosi cha kufanya ili usiwe mpweke, Tembelea mbuga za wanyama au nenda
nchi nyingine kama una uwezo na jifunze vitu vipya.
Jenga ukaribu na Marafiki zako
Inasemekana kuwa marafiki wengi hupoteana au huwa hawana tena mazoea
ya karibu pindi wanapoanza mahusiano, angalia umeshakuwa mbali na
marafiki zako wangapi toka uanze mahusiano na jenga tena urafiki na watu
wako.
Zingatia kusubiri kabla hujaanza mahusiano mapya, unaweza kujiingiza
kwenye mahusiano mengine ambayo yatakuwa matatizo kuliko ulipotoka na
ukajikuta unajutia maamuzi yako.
No comments:
Post a Comment