Kupitia account yake ya mtandao wa twitter,staa wa miondoko
ya Afro-Pop ambae pia ni Host wa show ya “Lip Sync” inayorushwa na
kituo cha televisheni cha MTv,D’Banj amedai kuwa yupo mbioni kuifikisha
mahakamani moja ya kampuni inayomiliki mtandao wa simu nchini Nigeria
kwa madai ya kampuni hiyo kujinufaisha kibiashara kupitia kazi zake za
kisanaa bila kuzingatia makubaliano na hakimiliki ya kazi hizo.

Hata hivyo kampuni inayotuhumiwa na Mwanamuziki huyo inatajwa kuwa ni
Globacom,kampuni
ambayo D’Banj alikua balozi wake ambapo tangu mkataba wake ulipoisha
kama balozi wa mtandao huo,hajasaini mkataba na kampuni nyingine.

Hatua
ya Mwanamuziki hiyo imekuja ambapo pia tarehe 4 ya mwezi May mwka
huu,alitangaza kusitisha mkataba wake kama balozi wa kinywaji cha “Ciroc
Vodka”huku tetesi zikidai kuwa yupo kwenye mpango wa kuzindua brand ya
kinywaji chake binafsi.

D’banj & Kanye West.
No comments:
Post a Comment