Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu kati ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars umemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Elias Maguli alianza kuipa Stars bao la kuongoza kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri iliyopigwa na Juma Abdul.
Lakini baadaye Kenya walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Victor Wanyama anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Southampton inayoshiriki ligi kuu nchini England.
Mechi hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya vikosi hivyo kujipima nguvu kabla ya mechi zao kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017. Stars itakuwa mwenyeji wa Misri June 4, kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment