Wednesday, 18 May 2016

Mzee akabiliana na mamba kwa saa 3 Australia

mamba


Mzee mmoja wa miaka 72 amewaambia waokoaji vile alivyokabiliana na mamba alipomuona mwenzake akizamishwa na myama huyo ndani ya maji kaskazini mwa Australia.
Wawili hao walikuwa wakivua kaa wa matopeni wakati mamba mmoja alipozamisha boti yao ya uvuvi katika mkondo wa bahari wa Leaders mjini Darwin Jumanne asubuhi.
Mtu mmoja alizama baada ya kung'atwa na mamba huyo alipokuwa akijaribu kupanda boti hiyo.
Mvuvi mwengine alifanikiwa kumpiga mamba huyo spana katika kichwa katika kisa hicho cha saa tatu.
Msemaji wa ambyulansi ya angani Ian Badham alisema kuwa mamba hao waliendelea kumvamia mzee huyo wakati wa tukio hilo baya.

No comments:

Post a Comment