Wanadoa maarufu wamelazimika kulitoroka taifa lao la Iran kutokana na picha walizochapisha mtandaoni.
Chini ya sheria kali za Kiislamu nchini humo,wanawake ni sharti wafunike vichwa vyao wakiwa hadharani tangu mwaka 1979.Lakini mwanamitindo Elnaz Golrokh ambaye pamoja na mumewe Hamid Fadei ni watu maarufu sana nchini Iran kutokana na picha hizo walizochapisha katika mtandao wa Instagram,amekuwa akichapisha picha hizo bila kujifunika kichwa.
Na sasa wameanza kuweka tena picha zao baada ya kutorokea Dubai.
Wanamitindo wengi katika mtandao wa Instagram hawajifuniki kichwa licha ya kuwa kinyume na sheria.
Mamlaka inafikiri kwamba picha zinazochapishwa katika mitandao ya kijamii hazizingatii sheria za kiislamu,na kiongozi wa kidini nchini humo ameutaja mtandao kama vita vya magahribi dhidi ya mashariki.
No comments:
Post a Comment