Wednesday, 18 May 2016

Mke apigwa faini kwa kufungua simu ya mumewe

Simu


Mwanamke mmoja katika muungano wa milki za kiarabu amepigwa faini na kurudishwa kwao baada ya kupatikana akiingia katika faragha ya mumewe.
Vyombo vya habari vinasema kuwa mwanamke huyo alichukua na kufungua simu ya mumewe baada ya kumshuku kwamba alikuwa na uhusiano wa kando.
Mumewe alilalamika kwa maafisa wa polisi na mkewe akashtakiwa chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni, kulingana na chombo cha habari cha Gulf News.
Mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa na ambaye ni mgeni katika muungano wa milki za kiarabu alipigwa faini ya pauni 28,000.
Alikiri mahakamani kwamba aliifungua simu ya mumewe bila ya ruhusa na kuzituma picha katika simu yake wakili wake aliiambia Gulf News.
Wakili huyo Eman Sabt,alisema kwamba wanandoa hao walikuwa na umri wa miaka ya 30 na wenye asili ya kiarabu,lakini hakutoa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment