Adhabu ni sehemu ya maisha katika malezi
ya watoto lakini imekuwa tofauti kwa wazazi hawa kutoka Japan ambao
waliamua kumuadhibu mtoto wao mwenye umri wa miaka (7) Yamato Tanooka,
kwa kumuacha katika msitu wa kisiwa cha Hokaido ambapo ni makazi ya
wanyama pori baada ya kumkuta na kosa la kurushia mawe magari yaliyokua
jirani yao.
Kikosi cha waokoaji zaidi ya 150 bado kinaendelea na msako huko Nanae Japan
ikiwa leo ni siku ya tatu tangu apotee. Wazazi wa mtoto huyo wamekiri
kufanya hivyo ila haikuwa dhumuni lao kumuacha kwa muda mrefu kwani
walirudi eneo la tukio muda mfupi tangu wamuache ila walipofika
hawakumkuta.
Mwanzoni baba wa mtoto huyo aliripoti
kupotea kwa mwanae walipokuwa wanatafuta mboga, lakini baadae akaamua
kuwaambia polisi ukweli na kusema walimshusha kwenye gari kama kumpa
adhabu tu. Mpaka sasa polisi wanafikiria juu ya swala hili na huenda
wakafunguliwa kesi ya ‘Utelekezaji wa mtoto‘.
No comments:
Post a Comment